Jumanne , 19th Mar , 2019

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, amesema kwamba sababu iliyomfanya kukichagua chama cha ACT- Wazalendo ni pamoja na moyo wake kuridhia.

Zitto kulia akiwa pamoja na Maalim Seif

Amesema kwamba, kabla ya kufanya maamuzi walitembelea vyama vyote vinavyounda Ukawa ili kuchagua kipi kingemfaa yeye pamoja na wenzake na ndipo wakavutiwa na chama hicho.

Amesema baada ya kutazama vyama hivyo waliamua kukitembelea ACT na kwa kuwa tayari kilikwishapeleka maombi ya kujiunga na Ukawa ndipo mahali mioyo yao iliporidhia.

"Vyama vya upinzani vyote ni vizuri, lakini kwenye uzuri kipo ambacho kinazid. ACT mioyo yetu imeridhia safi kabisa", amesema.

Baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa ACT, Maalim amesema hataki kutajiwa au kusikia habari za Lipumba kwa kuwa hataki kugombana tena na kiongozi huyo.

Seif akijibu swali la kuhusu Lipumba kudai kwamba Seif alidekezwa ndani ya chama ndiyo maana yametokea yaliyotokea, amesema kwamba kwa upande wake na Lipumba yamekwisha

"Leo sitaki kuongelea lolote kuhusu Lipumba, sitaki kulumbana na yeye. Lipumba Kwangu mimi finish", amemalizi Maalim kwa msisitizo.