Alhamisi , 19th Apr , 2018

Waajiri ambao bado hawaja wasilisha majina ya wafanyakazi wao ambao ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu wametakiwa kufanya hivyo kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria dhidi yao kutokana na kupinga agizo.

Agizo hilo limetolewa Jijini Mwanza na mkurugenzi msaidizi wa uejeshaji mikopo wa bodi hiyo Fidelis Joseph ambapo amesema badhi ya waajiri hawajasilisha majina ya wafanyakazi wao kwenye bodi hiyo mpaka sasa.

Akiambatana na maafisa wa bodi hiyo Jijini Mwanza wametembelea Hospitali ya Uhuru Jijini humo na kukuta bado hawajawasilisha majina hayo kwenye bodi na kusema ni kosa la kisheria kukaidi amri na yoyote atakae jaribu kuzuia zoezi hilo kutekeleza katika shirika au kampuni yake basi hatua za kisheria zitafuata.

Kwa habari kamili msikilize hapa Mkurugenzi msaidizi wa mikopo ya elimu ya juu Fidelis Joseph.