Jumapili , 15th Sep , 2019

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema amefurahishwa na hotuba ya kuomba msamaha iliyotolewa na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, baada ya wananchi wa Zimbabwe kumzomea wakati wa zoezi la kuaga mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe

Makamu wa Rais Samia Suluhu amesema hotuba ya Rais wa Afrika ya Kusini Ramaphoser aliyoitoa kwa wananchi wa Zimbabwe na Afrika kwa Ujumla, ni kitendo cha ungwana kwa kuweza kuomba samahani, kutokana na vitendo vinavyoendelea kufanywa wa wananchi wa Afrika Kusini.

"Nimefurahishwa sana na hotuba aliyoitoa Rais wa Ramaphosa kwa sababu alipoanza wananchi walikuwa wanamzomea sana, lakini aliomba samahani kwa Afrika na samahani kwa Zimbabwe na wananchi walimpenda sana." amesema Makamu wa Rais

Hafla ya kumuaga Mzee Mugabe imefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Taifa wa Michezo Jijini Harare Nchini Zimbabwe ambapo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Magufuli kwenye.