Serikali kutoa matibabu ya bure ugonjwa huu

Jumatatu , 10th Jun , 2019

Serikali imesema imeandaa mpango wa kutoa matibabu ya bure kwa watoto watakaokuwa wakiugua ugonjwa wa Selimundu, kwa kupatiwa vibali maalum vya huduma bila malipo kufuatia kufanyiwa uhakiki kwa familia zisizojiweza.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndugulile, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Taska Mbogo, ambaye alihoji juu ya wagonjwa hao kupewa matibabu ya bure.

Mbunge amehoji kuwa "Serikali ina mpango gani kuwasaidia wagonjwa wa Sickle cell (Seli mundu) ili watibiwe bure?"

Akijibu swali  Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Ndugulile amesema kuwa "kupitia Wizara ya Afya tumeandaa muongozo wa kutoa msamaha kwa wagonjwa wa Sickle cell (Seli mundu), familia zisizojiweza zitahakikiwa na kupewa kibali cha huduma bila malipo. Serikali inaanzisha mpango wa taifa kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza."

Kwa sasa Bunge linandelea jijini Dodoma ambapo Mawaziri mbalimbali wameendelea kuwasilisha Makadirio yao ya Bajeti kwenye Wizara zao.