Jumatatu , 11th Feb , 2019

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Bunge, imepitisha sheria mpya kwaajili ya kodi ya nyumba ambazo zimejengwa kwenye eneo moja.

Rais Magufuli

Taarifa ya msemaji mkuu wa serikali Dkt. Hassan Abbas imeweka wazi juu ya mabadiliko ya sheria za kodi ambayo sasa itampa haki mmiliki wa nyumba zaidi ya moja katika kiwanja kimoja kulipia nyumba moja tu.

''Bunge limepitisha mabadiliko ya sheria za kodi, ambapo sasa kifungu cha 9(b) kinaainisha kuwa mtu akiwa na nyumba zaidi ya moja katika kiwanja kimoja atalipia nyumba moja pekee'', imeeleza taarifa ya Abbas.

Mbali na kodi hiyo pia serikali ipo kwenye mchakato wa kutengeneza sheria ambayo itawalinda wamiliki wa nyumba pamoja na wapangaji wao juu ya namna bora ya ulipaji kodi ikiwezekana kodi ilipwe kwa mwezi mmoja mmoja badala ya miezi sita hadi mwaka mmoja.