Jumamosi , 21st Jul , 2018

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Atashasta Nditiye ametengua katazo la wananchi kuzuiwa kupanda meli ya serikali hadi wawe na vitambulisho vya uraia au cha mpiga kura jijini Mwanza.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Atashasta Nditiye.

Nditiye amesema kuwa utaratibu wa awali uendelee kutumika hadi pale watakapo kaa upya kujadili ni njia ipi sahihi itakayoweza kuwawezesha wananchi kupata huduma ya usafiri bila kikwazo.

Nditiye ameongeza kuwa suala hilo lilitokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina ya Shirika la Meli pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama jijini humo.

Wananchi wanamatatizo mengi, unapoanza kumchanganya na mambo ya vitambulisho tena unakuwa unawavuruga naomba utaratibu wa awali utumike na tuangalie utaratibu mwingine hapo baadaye”, amesema Nditiye.

Mamia ya abiria waliotakiwa kusafiri kwa meli ya Mv.Nyehunge kutoka jijini Mwanza kuelekea wilayani Ukerewe wamekwama kwa siku nne katika bandari ya Mwaloni Kirumba jijini humo baada ya kushindwa kutekeleza sharti linalomtaka kila msafiri kuwa na kitambulisho rasmi cha uraia au kupigia kura.