Jumanne , 16th Apr , 2019

Naibu Waziri wa Sera Bunge Kazi, na ajira, Anthony Mavunde amesema mpaka kufikia Februari 28, 2019 Serikali ilishwalipa wastaafu 9971 waliokuwa wanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF ambao wamelipwa zaidi ya shilingi bilioni 888.

Naibu Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri Mkuu ambalo liliulizwa na Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga ambapo alihoji juu ya hatma ya wastaafu.

Mbunge Haonga ameuliza kuwa, "watumishi wa Halmashauri nyingi waliokuwa wanachama wa PSPF, wamestaafu kwa zaidi ya mwaka 1, hawajalipwa pesa zao, lini Serikali itawalipa?".

Akijibu swali hilo, Mavunde amesema, "mpaka Februari 28, 2019 mfuko mpya wa PSSF ulikamilisha malipo ya wastaafu waliorithiwa PSPF jumla yao ni 9971 na wamelipwa Bil.888, mfumo wa ulipaji wa mafao ndani ya Mkoa umekamilika, na utafanya mfuko kulipa ndani ya muda wa kisheria."

Kwa sasa Bunge la bajeti linaendelea jijini Dodoma ambapo Mawaziri wameenda kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka fedha 2019/2020.