Jumanne , 12th Nov , 2019

Serikali imewataka watu ambao hawaridhiki na mwenendo wa shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,  bado wanayo fursa ya kufungua kesi kwenye Mahakama za Afrika Mashariki au kushtaki katika Bunge la Afrika Mashariki.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro, wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni leo Novemba 12, 2019, jijini Dodoma, ambapo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa CUF, Ally Saleh.

Ally Saleh ameuliza kuwa "tabia ya kuwakata wagombea wa upinzani kwa zaidi ya asilimia 90, Tanzania inakiuka matakwa ya Afrika Mashariki?"

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Damas Ndumbaro, amesema kwa mujibu wa mkataba wa Afrika Mashariki, ambao wanaona mambo hayako sawa wanayo nafasi ya kwenda huko.

"Tanzania inafuata misingi ya utawala bora ya Afrika Mashariki, ambaye amekwazwa akalalamike Bunge au Mahakama za Afrika Mashariki." amesema Ndumbaro.

Kwa sasa Bunge linaendelea jijini Dodoma, ambapo wabunge mbalimbali wanauliza maswali na kujibiwa na Mawaziri.