Shibuda adai CCM inadhalilishwa

Jumamosi , 12th Jan , 2019

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Maswa kupitia CCM, na Maswa Magharibi, John Shibuda amesema Muswada wa Vyama vya Sheria unaotarajia kupelekwa bungeni unaidhalilisha CCM.

Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya Siasa, John Shibuda.

Akizungumza leo katika mdahalo wa vyama vya siasa, Shibuda kwa sasa ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya Siasa visivyo na uwakilishi bungeni, amesema CCM kama mzazi wa vyama vingi havipaswi kukandamiza vyama hivyo.

Akifafanua kuhusu kifungu kinachozuia viongozi kuhama vyama na kupewa nafasi za kugombea, Shibuda amehoji kwanini mwanachama azuiwe wakati ni ujuru wake na chama chake kufanya hivyo.

"Unamuogopa nani?, Inamaana ukihama dini moja labda umetoka Uislam kwenda Ukristo usioe mpaka mwaka upite?. Kasema nani? Sheria hii inaidhalilisha CCM. Nawaombeni mnaokwenda kutegeneza sheria mkazijadili kwa kina" Shibuda.

Aidha ameongeza kwamba, "Mzazi wa vyama vingi ni CCM na mlezi wake ni serikali. Sasa mzazi ukizaa mtoto ukamuacha akiwa chokoraa akikutukana usilalamike. Tengenezeni tafsiri ya huu muswada. Chama cha siasa kinapaswa kukonga nyoyo za wananchi na siyo kutegemea kuua chama kingine".