Jumapili , 31st Mei , 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Mh. Seleman Jafo ameonesha kufurahishwa na kazi kubwa ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Bweni ya wasichana aliyoipa jina la Jokate Girls High School iliyopo Mhaga wilayani Kisarawe.

Picha kubwa ni moja ya majengo ya shule ya Sekondari Jokate Mwegelo na picha ndogo ni DCJokate Mwegelo.

Waziri jafo amesema hayo alipotembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo ambayo inataraji kuanza muhula mpya wa masomo kwa wanafunzi wa kidato cha tano  wanaotaraji kuanza ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

''Hili jambo zuri na la kupongezwa kwa jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, na Mkurugenzi naomba uanze kushughulikia usajili wa shule hii 

Jafo amewataka wanaopewa dhamana ya kusimamia miradi inayotekelezwa na serikali kote nchini kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuliletea taifa maendeleo.

Akitoa taarifa kwa Mh. Waziri Jafo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama amesema mpaka ujenzi huo umefikia asilimia sabini huku ukitumia zaidi ya shilingi million mia tano za kitanzania zilizotokana na michango mbalimbali iliyochangishwa katika harambee ya Tokomeza Zero Kisarawe.

Tazama video hapa chini