"Sitaki kumuona Lipumba" - Mtolea

Wednesday , 12th Jul , 2017

Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Ally Mtolea amefunguka na kusema kwa sasa hana jambo la kumshauri Profesa Lipumba na kudai haitaji hata kumuona kwa sababu ameshapoteza ile heshima na thamani yake.

Mtolea amesema hayo leo alipokuwa akihojiwa na EATV na kusema yeye alikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanamuheshimu sana  Prof. Ibrahim Lipumba kiasi kwamba ilifika hatua hakutaka kua muongeaji sana juu ya mambo yake lakini kwa kuwa tayari ameshajivunjia heshima mwenyewe hivyo hana budi kusema.

"Mimi nilianza kuona nia mbaya ya Lipumba pale aliponikatalia kwenda kwenye ufunguzi wa kampeni zangu mwaka 2015 kwani nilimfuata lakini yeye alikataa kabisa, lakini niliposhinda ubunge nilimfuata pia na kumpa taarifa na kumuomba tuendelee kushirikiana nikiamini yeye ni mkongwe katika siasa kuna mambo mengi ya kunishauri na kuniongoza sikumtenga kabisa, ila aliposema anataka kurudi baada ya kujiuzulu mimi sikumuelewa ni nikamfuata nikimwambia mzee unataka kutuletea mgogoro" alisema Mtolea 

Mbali na hilo Mtolea anasema saizi Lipumba amefikia hatua ambayo haambiliki chochote na kusema hatamani hata kukutana naye 

Msikilize hapa akifunguka zaidi