Jumanne , 18th Feb , 2020

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Japhet Kibona, amesema kuwa mpaka sasa hawajajua chanzo cha moto ulioteketeza soko la Tegeta, yakiwemo maduka na vibanda vya nafaka na kwamba tathmini inaendelea kufanyika ili kujua ni hasara kiasi gani imepatikana.

Picha ikionesha jinsi Soko la Tegeta lilivyoteketea

Akizungumza na EATV &EA Radio Digital, Kamanda Kibona amesema kuwa tukio hilo la moto limetokea usiku wa kuamkia leo Februari 18, 2020.

"Moto usiku ulidhibitiwa lakini leo asubuhi tena ulishika kwenye vibanda Saba na sehemu ya mazao ya nafaka na wamefanikiwa kuuzima, tathmini ya kujua ni kibanda cha nani na ni hasara kiasi gani imetokea ndio inafanyika, na bado tunachunguza chanzo cha moto huo" amesema ACP Kibona.