Ijumaa , 18th Mei , 2018

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yuston Ndugai ameonyesha kufurahishwa na umoja waliouonyesha wabunge katika kuwaunga mkono wabunge waislamu katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Akionyesha furaha yake bungeni, Spika amesema kwamba amependa jinsi ambavyo wabunge wameonyesha umoja kwa kuvaa stara (Hijab) huku akimpongeza Naibu Spika Tulia Ackson kaongoza kwa kwa kufunika.

"Waheshimiwa wabunge tunaendelea lakini kabla hatujaendelea, kwa utafiti wangu niliofanya leo watu humu ndani wamependeza kwa kuvaa bargashia na kanzu. Hongereni sana, lakini tukumbuke kanuni tunapovaa lazima tuvae inavyotakiwa kama kule pwani na miguuni siyo kuvaa kiatu cha kamba, bali kobazi" Spika.

Ameongeza "Kwa upande wa kina mama leo Hijab zimekubali. Lakini katika hijab,  hijab namba moja leo hii ni ya Naibu wangu Mhe. Naibu Spika (huku akicheka) na hii inaonyesha utanzania wetu jinsi ambavyo sisi ni wamoja".