Jumatatu , 18th Nov , 2019

Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Pius Msekwa, amesema anaunga mkono kauli ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kupitia kitabu chake cha 'My Life My Purpose', kuwa baadhi ya wagombea wa upinzani kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, walikuwa na hoja dhaifu na kupelekea Rais Mstaafu Mkapa kupata

Benjamin Mkapa

ushindi kwenye Uchaguzi huo.

Pius Msekwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital, iliyotaka kufahamu kuhusiana na maoni yake juu ya Kitabu kilichozinduliwa na Rais Mstaafu Mkapa, ambapo miongoni mwa mambo aliyoyaeleza kwenye kitabu hicho kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa 1995 ni kuwa wapinzani wake walikuwa dhaifu kwa hoja.

Pius Msekwa amesema kuwa "Kiukweli hata mimi ninachokikumbuka ndiyo kile ambacho amekisema Mkapa, ila yeye amepata muda zaidi wa kuangalia mambo aliyokutana nayo, niwasihi tu vijana kasomeni yale ya kwenye Kitabu na muyazingatie kabisa."

Novemba 12, 2019 ikiwa siku yake ya kuzaliwa Rais Mstaafu Mkapa, alizindua kitabu chake alichokiita kwa jina la 'My Life, My Purpose', ambapo viongozi mbalimbali wa Kitaifa walishiriki, akiwemo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete pampja Ali Hassan Mwinyi.