Spika Ndugai azuia 'Kigogo' kutajwa Bungeni

Ijumaa , 5th Jun , 2020

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amewazuia Wabunge ndani ya Bunge hilo kutaja jina la Kigogo.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.

Spika Ndugai ameyabainisha hayo leo Juni 5, 2020, wakati Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, akichangia hoja ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo na ndipo alipotolea mfano wa baadhi ya watu kwamba wamekuwa wakikamatwa na kutakiwa kumtaja mtu anayetumia jina la Kigogo katika mtandao wa Twitter.

Mbunge Lema alisema kuwa"Waacheni watu mitandaoni wapumue, wanachosema kama siyo ukweli Waziri atoke ajibu, nyie mnasemwa sababu ni Serikali, na sisi tukiwa Serikali tutasemwa kwa kiwango chenu, mimi siyo Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa sasa waniseme kwa kipi, sasa Mheshimiwa Spika mkiwazuia nini kinatokea, siku hizi watu wengi wanakamatwa Kigogo ni nani Kigogo ni nani".

Mara baada ya Mh Lema kutoa kauli hiyo, Spika Ndugai akajibu, "Aaah nimepiga marufuku, huyo achana naye".