Sugu amtaka JPM kuongeza mishahara

Ijumaa , 12th Apr , 2019

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amemtaka Rais Magufuli atakapofika Mbeya kwa ajili ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma kwa sababu miaka yake minne hajawahi kuongeza hata kidogo.

Mbilinyi ametoa kauli hiyo wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo amesema anamuomba Rais atakapokuwa Mbeya aongeze mishahara kwa wafanyakazi.

Wafanyakazi wana hali mbaya sana maeneo yote ya nchi hii. Rais aangalie suala la wastaafu wengine ni mwaka wa pili sasa hawajalipwa mafao yao, katika idara za ulinzi na usalama kama Magereza, Polisi ni miaka miwili wastaafu wapo kota hawana nauli za kubebea mizigo kurudi kwao”.

Rais amesema Watanzania si wajinga kwa tukio la Mohammed Dewji, pia Watanzania wanajiuliza kuhusu Tundu Lissu na Ben Saanane uchunguzi unaendeleaje”, ameongeza Mbunge Sugu.

Sugu ni miongoni mwa Wabunge 10 wa Bunge la Tanzania ambao kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 walishinda kwa kura nyingi, aliwahi kufungwa jela miezi 5 kwa makosa ya kutoa kauli za uchochezi lakini baadaye aliotolewa kwa msamaha wa Rais.