Ijumaa , 20th Apr , 2018

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Mtwara imesema hairidhishwi na adhabu zinazotolewa kwa wanaokutwa na hatia kwa makosa mbalimbali ya rushwa kutokana na vifungu vya sheria kuainisha adhbu ndogo ukilinganisha na ukubwa wa kosa.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Stephen Mafipa, ameeleza hayo wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa tayari wamepeleka mapendekezo makao makuu kwa ajili ya kushughulikia maboresho ya sheria hizo.

Aidha, kamanda huyo wa TAKUKURU amezitaja taasisi zinazoongoza kwa kulalamikiwa juu ya makosa ya rushwa kuwa ni pamoja na vyama vya ushirika ambavyo jumla ya malalamiko 24 yamewasilishwa.

Taasisi hiyo imesema katika kipindi hicho jumla ya kesi 25 ziliendelea Mahakamani katika mkoa wa Mtwara na wilaya zake, ambapo taasisi zinazoongoza kwa ni pamoja na halmashuri kesi 19.