Jumanne , 26th Nov , 2019

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Mbungo, amezitaka taasisi na mashirika yote yaliyotafuna fedha za vyama vya Msingi na Ushirika kuzirudisha haraka iwezekanavyo kuanzia leo Novemba 26, na kwamba wasipofanya hivyo watafikish

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Mbungo, akikabidhiwa ripoti na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga.

 

na kutaifishwa mali zao.

Hayo ameyabainisha wakati akipokea muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa Vyama vya Ushirika, uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa Serikali ulioko Mtumba Jijini Dodoma.

"Natoa rai kwa wale wote wana Ushirika, Bodi za Ushirika na wote waliokuwa wanakusanya fedha za Saccos, waanze kurudisha fedha hizo kuanzia leo, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao tutawachunguza na hatutaacha jiwe lolote ambalo halijageuzwa kwenye hilo suala la Ushirika" amesema Brig Jenerali Mbungo.

Aidha Jenerali Mbungo ameongeza kuwa "Ubadhirifu wowote haukubaliki kwani ni wizi kama wizi mwingine, endapo hawatarudisha sisi uchunguzi tutauanza mara moja pale ambapo kutakuwa na ushahidi hatua kali zitachukuliwa ikiwemo kupelekwa mahakamani, lakini hata kabla ya kushtakiwa kwa kushirikiana na Mwendesha Mashtaka wa Serikali tutapeleka maombi ya kutaifishwa mali walizonazo" ameongeza.

Kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019, Serikali ilitoa maagizo kwa Shirika la COASCO kukagua Vyama vya Ushirika vyote, ambapo hadi tarehe 30 Juni, 2019 Vyama vya Ushirika vilivyosajiliwa vilikuwa 11,410, kati ya Vyama hivyo, Vyama hai ni 6,463, Vyama Sinzia ni 2,844 na Vyama ambavyo havipatikani 2,103.

Kutokana na maagizo hayo, hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2019 COASCO ilikagua Vyama vya Ushirika vipatavyo 4,413 sawa na asilimia 102.63 ya lengo la Serikali la kukagua Vyama 4,300.

Katika vyama hivyo 4,413 vilivyokaguliwa, vyama 303 (6.87%) vilipata Hati inayoridhisha, vyama 2,378 (53.89%) vilipata Hati yenye shaka, vyama 879 (19.92%) vilipata Hati isiyoridhisha na vyama 853 (19.32%) vilipata Hati mbaya.