Ijumaa , 11th Sep , 2020

Diane Downs mwanamke kutoka Marekani aliyetajwa kuwa miongoni mwa wanawake katili sana, tukio lake la kwanza la Mei 1983 ndilo lililoacha watu midomo wazi, inaelezwa kuwa alijaribu kuwaua watoto wake watatu wa kuwazaa, taarifa zinasema kuwa alifanikiwa kumuua mmoja huku akiwajeruhi vibaya.

Wanawake wanaodaiwa kuwa makatili zaidi.

watoto wawili waliobakia na hakusema sababu iliyokuwa na maana katika utetezi wake

Mwanamke mwingine ni Genene Jones kutoka nchini Marekani, mwenye kibali cha uuguzi katika Jimbo la Texas, uhatari wa mwanamke huyo unakuja pale ambapo alifanya mauaji ya vichanga zaidi ya sitini pamoja na watoto kadhaa chini ya uangalizi wake mnamo mwaka 1970 hadi 1980, inaelezwa kuwa mauaji aliyafanya kwa kuwachoma watoto hao sindano zenye dawa kali aina ya Heparin, na baadaye alikutwa na hatia hiyo na kuhukumiwa kifo.

Erna Petri ni mwanamke kutoka nchini Ujerumani alizaliwa 1920, miongoni mwa tukio la kinyama zaidi alilowahi kufanya ni kuchukua watoto sita waliokuwa njiani kutoka katika kambi ya Sobibo na kuwapeleka nyumbani kwake kisha kuwapa chakula, baada ya hapo aliwapeleka kwenye kichaka kilicho jirani ya nyumba yake na kuwapiga risasi.

Mwingine ni Johanna Altvater alizaliwa mwaka 1920, aliwahi kuwa katibu katika chama cha Nazil cha nchini Ujerumani, inaelezwa kuwa mwanamke huyo ukatili wake ulikuwa ukiwalenga zaidi watoto wa kiyahudi katika matukio yake ya kinyama, watoto walikuwa wakimuamini kutokana na kuwapa zawadi mbalimbali  na baadaye alikuwa akiwakusanya na kuwaua.

Nannie Doss kutoka Marekani alikuwa akifahamika kwa majina mengi miongoni mwa jina lililo muelezea zaidi ni jina la Black Widow, alikuwa ni hatari na aliolewa na wanaume wanne na wote aliwaua kutokana na sababu mbalimbali, baadaye ilibainika kuwa alihusika pia katika mauaji ya dada zake wawili, watoto wake wawili, mama yake mzazi pamoja na Mama mkwe wake na baadae alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani mwaka 1954.

Watafiti wanasema kuwa ipo idadi kubwa ambayo haijabainika kuhusiana na wanawake makatili zaidi Duniani .