Alhamisi , 18th Jul , 2019

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imekifuta Chuo Kikuu cha Eckernforde cha mkoani Tanga kutokana na chuo hicho kushindwa kukidhi vigezo vya udahili.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa, ambapo amesema licha ya kukifuta chuo hicho, pia vyuo ambavyo havijatimiza vigezo vimepewa miezi sita ya kufanya hivyo ili viweze kufunguliwa.

''Tumekifuta chuo cha Eckernforde, sio tena Chuo Kikuu hapa Tanzania'', amesema Profesa Kihampa.

TCU imekifuta chuo hicho ikiwa ni miezi takribani kumi imepita tangu Septemba 25,2018, ilipotangaza kusitisha utoaji mafunzo na kuamuru wanafunzi waliokuwa wakisoma chuo hicho kuhamishiwa vyuo vingine.