Teddy Mapunda afariki dunia

Jumatano , 5th Mei , 2021

Mjasiriamali maarufu na mdau mkubwa wa vyombo vya habari Teddy Mapunda, amefariki dunia usiku wa jana Mei 4, 2021.

Teddy Mapunda enzi za uhai wake

Taarifa za awali zimeeleza kuwa aliugua ghafla wakati akipata futari na wenzake katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kukimbizwa hospitali ya Aga Khan, ambapo alifariki dunia.

Mbali na vyombo vya habari, Teddy pia alikuwa mdau mkubwa wa michezo na mjumbe wa kamati ya saidia Taifa Stars ishinde.

Tutaendelea kukupatia ratiba zaidi za msiba huo.