''Tuache balaa, ugomvi, fitina'' - Mzee Mwinyi

Jumatatu , 12th Apr , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Mzee Ali Hassan Mwinyi, alifika kumsalimia Rais Samia Nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Aprili, 2021.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya mazungumzo hayo, Mzee Ali Hassan Mwinyi amesema ''Tumepata Rais mpya, kijana tena mwanamke kwahiyo sisi wazee tunakuja kudeka''.

Aidha Mzee Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuacha mambo yote na kuwa na umoja na mshikamano ili kusonga mbele chini ya Rais mpya Mhe. Samia Suluhu Hassan.

''Tumsaidie tuache balaa, tuache ugomvi, tuache fitina, upatikane umoja, tushikamane tuendelee,'' amesema.

Tazama Video hapo chini