Jumatano , 11th Jan , 2017

Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania kimesema kinachofanyika hivi sasa ndani ya chama hicho ni mageuzi na wala siyo mabadiliko ya kawaida, kwa kuwa mageuzi ni zaidi ya mabadiliko, lengo likiwa ni kuwa chama makini cha siasa kwa ajili ya maendeleo.

Humprey Polepole - Katibu wa Itikadi na uenezi CCM

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole, amesema katika mageuzi yatakayofanyika hivi sasa ndani ya chama hicho yatagusa maeneo matatu ambayo ni pamoja na eneo la uongozi kwa kuweka viongozi waadilifu, eneo la pili ni mfumo ili chama kiwe na tija, na eneo la tatu ikiwa ni utawala. 

Msikilize hapa Polepole akifafanua hatma ya chama hicho wakati akifanya mahojiano na East Africa Radio, wakati akiwa Kikaangoni ya EATV.......