'Tunatafuta kauli tata za uchochezi' - Mabeyo

Jumamosi , 13th Apr , 2019

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amesema jeshi la Wananchi wa Tanzania linafuatilia kauli tata zinazoashiria uchochezi kuharibu amani ya Tanzania.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo.

Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Mji wa Serikali uliopo Dodoma wilaya ya Chamwino ambapo amesema jeshi hilo halitamvumilia anayetaka kuchafua amani ya Tanzania.

"Ndani ya nchi yetu kwa kushirikiana na vyombo vingine tutawalinda wananchi na mali zao, tutakabiliana na matishio ndani ya nchi yetu, na sasa hivi tunaendelea kufuatilia kauli tata zinazoashiria uchochezi na machafuko ndani ya nchi yetu" amesema Mabeyo

Aidha katika hafla hiyo Rais Magufuli amesema "wanaomaliza JKT ndiyo waajiriwe kwenye Majeshi yetu sasa ipitie orodha vizuri kama ni 1000 na hawazidi 1500 wote nawaajiri lakini wasiongezwe wengine"