Tundu Lissu aikataa nafasi ya U-makamu wa rais

Alhamisi , 14th Mar , 2019

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu amesema hana mpango wa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi, hivyo anastahili kuendelea kupatiwa stahiki zake za ubunge zikiwepo posho na mshahara.

Mbunge Tundu Lissu

Lissu amesema hana mpango wa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi, hivyo anastahili kuendelea kupatiwa stahiki zake za ubunge zikiwepo posho na mshahara.

Lissu aemeyasema hayo wakati akielezea vifungu vya sheria vilivyopo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba katika Ibara ya 71, moja ya jambo ambalo litamfanya Mbunge kukoma kupatiwa stahiki zake ni pale anapoteuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi.

Jana Februari 13,  Lissu amethibitisha kuwa uongozi wa Bunge kupitia kwa spika, Job Ndugai na katibu wake Steven Kagaigai umemfutia rasmi mshahara na posho za kibunge kwa kile alichoeleza kuwa ofisi ya spika haina taarifa za anachokifanya nje ya nchi.

"Katika Katiba ya nchi, Ibara ya 71 kati ya sababu zilizotajwa na ibara hiyo, sababu ya sita inasema endapo ukiteuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa rais, hutapata stahiki za kibunge. Mimi sitajii kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais", amesema.

Pamoja na sababu mbalimbali alizozitaja Mbunge huyo zitakazopelekea kunyimwa stahiki zake za Kibunge amesema hakuna sababu yoyote inayomfunga hivyo Bunge linapaswa kumpatia stahiki zake kwani kama ni kutokuwepo kwake bungeni, Spika Ndugai alikuwepo katika kikao kilichoadhimia yeye apelekwe Nairobi kwa matibabu wakati alipokuwa hoi baada ya kupigwa risasi Septemba 07, 2017.

Mbali na hayo Lissu amesema ameshawasiliana na wanasheria wake walipo Tanzania waweze kufungu mashtaka dhidi ya Bunge kwa kuzuia mishahara na posho zake.