Jumatatu , 18th Mar , 2019

Hatua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kuhama chama chake cha muda mrefu na kuhamia ACT - Wazalendo, imeonekana kumuweka kwenye wakati mgumu mbunge Ally Saleh ambaye ni miongoni wafuasi wake.

www.eatv.tv ilimtafuta Mbunge huyo wa Malindi Visiwani Zanzibar, ambaye ni miongoni mwa wabunge ambao walikuwa upande wa Maalim ili kufahamu msimamo wao baada ya Maalim Seif kuhama chama.

"Mimi siwezi kuongea chochote kwa sasa, nitaweza kuzungumzia suala hilo baada ya siku 2" amesema Mbunge wa Malindi Ally Saleh.

Mapema leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.

Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama majira ya saa nane leo Machi 18, 2019, alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT- Wazalendo kwa kile alichokidai amesoma katiba za vyama vingine na kubaini masharti ya chama hicho ni nafuu zaidi.