Ijumaa , 12th Apr , 2019

Serikali ya Ufaransa imesema kuwa suala la haki za binadamu, uhuru wa kujieleza pamoja na ushirikishwaji wananchi vikizingatiwa vitasaidia katika kuleta maendeleo zaidi kwa nchi ya Tanzania.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier akiwa na Spika Job Ndugai siku alipomtembelea jijini Dodoma

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier wakati alipokutana na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari katika mazungumzo ya pamoja.

Balozi Clavier amesema serikali yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, mazingira, afya na miundombinu lengo ni kuongeza upatikanaji wa huduma kwa jamii.