Jumapili , 20th Oct , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewataka vciongozi aliowaapisha leo Ikulu kuwa wavumilivu na wasihofie kuchafuliwa na watu, bali wajikite zaidi kwenye kutekeleza wajibu wao kama watumishi wa Umma.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na Balozi, ambapo kazi ya uongozi inahitaji uvumilivu.

"Kazi za uongozi zinahitaji uvumilivu, zinahitaji kumtanguliza Mungu mbele, utasemwa, utachafuliwa lakini ndiyo kazi ya uongozi, naombeni katimizeni wajibu wenu kaangalieni haki, kaangalieni sheria kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote" amesema Rais Magufuli

"Kazi hizi ni lazima tuwatumikie wananchi wanyonge, juzi nilikuwa Mtwara kaimu wa TAKUKURU anafahamu  tulikuta malalamiko kuhusu kulipwa korosho,baada ya kumuagiza amekuta vyama ushirika 32 vilivyokuwa vinawadhulumu , wananchi wameibiwa Bil. 1. 2" amesema Rais Magufuli