Ijumaa , 23rd Feb , 2018

Video Vixen maarufu bongo anayefanya poa kwa sasa na biashara yake ya urembo 'Nai' amefungukia sababu zilizomfanya kuachana na hit maker wa 'Ngarenaro' Dogo Janja ni baada ya mwanamuziki huyo kurudi upya kwenye chat na kumpotezea.

Nai amefunguka hayo akiwa kwenye mahojiano maalum ya msimu wa Valentine na kipindi cha Planet Bongo ya EATV, ambapo amedai kwamba baada ya msanii huyo kurejea kwenye muziki 2016 na ngoma ya My Life alianza kuwa bize na hata mawasiliano yakapungua kiasi ambacho kilimfanya ajisikie vibaya na kumuomba waachane.

"Mimi na Dogo Janja tulikuwa wapenzi kweli kipindi alivyorudi rasmi kwenye muziki nikaona kama anaanza kunipotezea. Mara yupo bize mawasiliano siyo kama mwanzo. Zikaanza drama nikasema ngoja nikae pembeni maana mimi siyo maarufu kama yeye,". Nai

Mbali na hayo, Nai amesema kwa sasa yeye na mwanamuziki huyo wamebaki kuwa kama marafiki na wanaishi kama hakikuwahi kutokea kitu kwani kila mmoja kwa sasa anamahusiano mengine mapya.

Kwa sasa mrembo huyo anayependezesha  video za wasanii mbalimbali ameweka kutoka kimahusiano na msanii anayeiwakilisha Dodoma vizuri 'Moni Centrozone'