Jumatatu , 8th Jun , 2020

Vifaa mbalimbali ambavyo bado havijafahamika thamani yake vimeibwa na hivyo kuathiri utoaji wa huduma za afya katika Zahanati ya Kawe Jijini Dar es Salaam katika kipindi ambacho ilikuwa haina uzio.

Zahanati ya Kawe

Hayo yamebainishwa leo na Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Vera Mlaki wakati wa kukabidhi rasmi mradi wa ujenzi wa uzio uliojengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Diwani wa kata hiyo, Muta Rwakatare.

Hafla hiyo ilienda sambamba na kukabidhi vitu mbalimbali ikiwemo vitanda na magongo ya kutembelea wagonjwa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu Manispaa ya Kinondoni, Dkt. Samwel Laizer ameeleza kuwa hatua mbalimbali zimechukuliwa na Serikali katika kuiboresha Zahanati hiyo kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa.