Ijumaa , 22nd Jun , 2018

Mwenyekiti wa Kavazi cha Mwl. Julius Kambarage Nyerere Prof. Issa Shivji amewashauri vijana kujenga utamaduni wa kujua historia ya nchi yao ikiwemo kufahamu masuala mbali mbali ambayo Baba wa taifa aliyafanya katika kupigania uhuru wa Tanzania.

Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere

Prof. Shivji ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa maonesho ya picha mbali mbali za baba wa Taifa yanayofanyika kwenye nyumba ya baba wa taifa iliyopo Magomeni ambayo aliitumia nyumba hiyo kuishi na kufanya shughuli za siasa na kupigania uhuru.

Prof Shivji amesema Vijana wengi hawana historia nzuri ya namna Mwl. Nyerere alivyopigania uhuru wa Tanzania, hivyo kwa kutembelea maonyesho hayo wataweza kukutana na picha mbalimbali ambazo zilitokana na namna yeye alivyokuwa akipagania uhuru wa nchi.

Kwa upande wake Muhifadhi Mkuu wa nyumba ya makumbusho ya Baba wa Taifa iliyopo Magomeni Bi. Neema Mbwana amesema kama vijana wataweza kuyatumia maonyesho ya siku tatu ambayo yataambatana na mijadala wataweza kuifahamu vizuri historia ya nchi yao katika kujiletea ukombozi.