Jumatatu , 21st Oct , 2019

Serikali wilayani Kilombero mkoani Morogoro imevionya baadhi ya vyama vya siasa, kuacha mara moja kutoa vitisho kwa wanachama na viongozi, ambao wamehama na kujiuzulu kwenye vyama vyao, kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama wakidai kuwa wanapokea taarifa za vitisho.

Nembo za vyama mbalimbali vya siasa

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo, wakati wa mkutano na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapo, kwa ajili kujadili changamoto zinazowakabili, ambapo amesema kuwa amepokea taarifa za baadhi ya wanachama ambao wamehama vyama vyao kutishiwa usalama wao.

Kwa upande wake aliyekuwa Diwani wa kata ya Katindiuka kupitia CHADEMA, Furaha Mganya, amesema kuwa amesikitishwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimfuatilia na kutaka kujua kwanini amejiuzulu nafasi yake na kuhamia CCM.

Kwenye mkutano huo Mbunge wa viti maalumu kupitia (CCM) Dkt Gertrude Rwakatare, amegawa baiskeli 300 zenye thamani ya shilingi milioni 45, kwa watendaji wa CCM wilayani Kilombero ili kuwarahisishia watendaji hao utakelezaji wa majukumu yao, huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, Novemba 24 mwaka huu.

Zaidi Tazama Video hapo chini.