Jumamosi , 16th Feb , 2019

Serikali ya Mkoa wa Manyara imewataka wachimbaji wadogo wa migodi ya madini ya Tanzanite yaliyopo Mererani wilayani Simanjiro mkoani, kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu utoroshaji wa madini ya Tanzanite kutokana na taarifa hizo kuisababishia hasara Serikali inapozifanyika kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti alipokuwa akipokea maandamano ya amani ya wachimbaji wadogo waliokuwa wakimpongeza Rais kwa kupunguza baadhi ya kodi zilizokuwa kero kwao katika mchakato mzima wa uchimbaji na uuzaji wa madini ya Vito.

Akizungumza na wananchi, wachimbaji, madalali pamoja na viongozi wa Chama Cha Wachimbaji madini mkoani humo (MAREMA), Mkuu wa Mkoa wa Mnyeti amewataka wachimbaji hao kuacha kulazimisha njaa zao kuwa njaa za taifa.

Kwa upande wao baadhi ya wachimbaji wakubwa kwa wadogo wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya Tanzanite One, Faisal Juma na mbunge wa Simanjiro James Milya wakitoa salam zao kwa kusema dhamana aliyoitoa Rais Magufuli kwao wataichunga na kuienzi kwa kulipa kodi stahiki kikamilifu .

Katika muswada  uliopelekwa bungeni kwa hati ya dharura kwa ajili ya marekebisho ya sheria ya madini baadhi ya tozo zilizoondoleea ni kodi ya huduma asilimia 5 na kodi ya ongezeko la thamani asilimia 18 ili kuleta ahuweni kwa wafanyabiashara ya madini