Alhamisi , 29th Sep , 2022

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imekutanisha wadau wa vifungashio, wazalishaji, wauzaji, wanunuzi na taasisi wezesheji katika uwanja wa maonesho wa Mwl. J.K. Nyerere  (Sabasaba) Dar es Salaam kujadili namna ya kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa M. Khamis

Akizungumza baada ya mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa M. Khamis, amesema kuwa kuna changamoto nyingi za upatikanaji wa vifungashio bora kwa bidhaa zinazozalishwa nchini, hivyo, TanTrade pamoja na wadau wengine serikalini na sekta binafsi  itaendelea kushirikiana ili kutatua changamoto ambayo inarudisha nyuma ushindani wa bidhaa zinazozalishwa nchini katika masoko ya ndani na nje.

Kwa upande wake msimamizi wa kituo cha vifungashio na ufungashaji Antonia Masoi, amesema kuwa mkutano huo ni muhimu sana katika kuwezesha bidhaa za wajasiriamali kuweza kushindana sokoni.