Jumanne , 11th Aug , 2020

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba na mgombea mwenza  Hamida Abdallah Huweishi, leo Agosti 11, 2020, wamechukua fomu zakugombea Urais katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo Dodoma.

Mgombea wa Urais kupitia CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akikabidhiwa fomu na M/Kiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistolces Kaijage.

Lipumba amewasili katika ofisi za NEC, mapema asubuhi leo, ambapo yeye na mgombea mwenza wamekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistolces Kaijage.

Mgombea mwingine aliyechukua fomu hii leo ni David Daudi Mwaijojele, kutoka chama cha CCK, ambaye alifika ofisini hapo akiwa mwenyewe bila mgombea mwenzake.

Zoezi la uchukuaji wa fomu hizo limeanza Agosti 5, 2020, na litafikia tamati Agosti 25.