
Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu
Waziri Ummy amesema lengo la kutoa agizo hilo ni kuhakikisha wanaondoa vikwazo vinavyoweza kupelekea mtoto kushindwa kuanza masomo yake kwa wakati.
"Nimesema kama January 17 imefika mwanafunzi hana sare za shule aruhusiwe kuingia darasani, mpe mzazi wiki 2 au mwezi, sijasema kwamba mtoto asiingie na uniform mwaka mzima, tunachotaka ni kuondoa vikwazo visivyo vya lazima kwa watoto wetu kupata elimu," afafanua Waziri Ummy.