Jumatatu , 19th Sep , 2022

Wanajeshi 250 wa Ukraine ambao wapo kwenye mpango wa majeshi ya kulinda amani ya umoja wa mataifa huko katika Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo DRC,  wamerejea nchini mwao. 

Lengo la kurejea nchini mwao ni kusaidia mapambano dhidi ya vikosi vya Russia.

Mwezi  March mwaka huu ilitanngzwa kwamba majeshi hayo yangerejea Ukraine huku onyo kutoka UN likisema kwamba ni hatari kwa usalama ikiwepo pia kuleta upungufu mkubwa wa rasilimali haswa  helikopta.

Mapambano dhidi ya vikosi vya waasi wanaoipinga serikali ambao wapo kwenye misitu minene ya mashariki kwa Congo ni muhimu sana kwa sasa.

 Helkopta 8 kutoka Ukraine huwa zinaunda  sehemu kubwa ya majeshi ya kulinda amani ya umoja wa mataifa  .

Tangu uvamizi wa majeshi ya  Russia nchini Ukraine  mwezi februari mwaka huu, nchi hiyo imekua kwenye mpango wa kuondoa  majeshi yake kutoka kwenye vikosi vya umoja wa mataifa kwenye maeneo mbalimbali .