Alhamisi , 22nd Aug , 2019

Wakati uandikishaji wa vitambulisho vya taifa ukiendelea, baadhi ya wananchi ambao wamepata vitambulisho katika maeneo mbalimbali na kukuta jina moja ua mawili yamekosewa, wameonekana kuchanganyikiwa baada ya kusikia kuwa watatakiwa kulipia shilingi elfu ishirini za kitanzania.

Kitambulisho cha mfano cha Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete

East Africa Drive baada ya kupata malalamiko hayo kutoka kwa baadhi ya wananchi, walifanyia kazi kwa kumtafuta Msemaji wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, Thomas William ambaye amesema, “Utaratibu ni kwamba kitambulisho kikikosewa majina au hata tarehe na mwaka wa kuzaliwa, kuna fursa ya kubadilisha kwani kinacholengwa ni kuwa na taarifa sahihi za mtu".

"Kuhusiana na malipo ni kwamba mtu atatakiwa kulipa elfu ishirini kama muombaji mwenyewe anataka kubadilisha majina yake mara baada ya kubadili dini au kwa namna yoyote vile lakini napo lazima afuate taratibu za kubadili majina”, ameongeza Thomas.

Msikilize zaidi hapo chini;