Alhamisi , 8th Dec , 2022

Mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya rufaa  mnazi mmoja Dr, Muhidini Abdi Mahmoud amelaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo vya kuwaondoa wagonjwa kimagendo hospitalini hapo kwa madai kuwa hakuna vifaa vya matibabu husika

Inaelezwa kuwa wagonjwa haohupelekwa  katika hospitali binafsi kwa lengo la kuwapatia matibabu kwa kuwatoza fedha

Hilo limebainika mara baada ya mkurugenzi huyo kubaini kutokuwepo kwa mgonjwa wa ajali ambae alikuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mnazi mmoja katika harakati za kumtafuta mgonjwa huyo alibainika kuwepo katika hospitali ya Aasiahh S Hospitali ilipo shehia ya mkele  mkoa mjini magharibi

Aidha Dr Muhidini amesema kufanya hivyo kwa madaktar hao ni kurudisha nyuma juhudi  za serikali kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika sekta ya afya ili kuhakikisha wanachi wanapatiwa matibabu huku akibainisha kua wahusika wote watachukuliwa hatua za kisheria