Jumatatu , 20th Jul , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema inategemea kuandikisha wapiga kura zaidi ya 2,900,00 katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR katika Mkoa wa Dar es Salaam, zoezi litakaloanza Julai 22 na kumalizika Julai 31 mwaka huu.

Akiongea leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Said Meck Sadik amewataka watu wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki katika kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Sadiki amewaka wananchi kutoa taarifa zao sahihi na kuepuka udanganyifu wowote huku akiwataka waandishaji kutobadilisha taarifa za mtu yoyote na atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Amesema maandalizi yamekamilika ambapo jumla ya vituo 1684 vimeandaliwa kutumika katika zoezi hilo na kwamba kila kituo kitakuwa na BVR Kits Operators 2 na mwandishi msaidizi 1 na kila kata kutakuwa na BVR Kits Operators 4 na waandishi wasaidizi 4 wa akiba.

Wakati huo huo Mecky Sadik amewataka wanasiasa kutoingilia zoezi hilo na maelekezo kuhusiana na mchakato wakati wa uandikishaji yatatolewana na Maafisa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi pekee na si vinginevyo.