Wataka somo la ngono kuwekwa kwenye mtaala

Jumanne , 13th Mar , 2018

Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti maendo ya ngono Dr. Annette Kezaabu, ameishauri serikali nchini Uganda kupitia wizara ya Elimu na michezo, kuingiza somo la filamu za ngono (pornography) kwenye mtaala wa shule za msingi na sekondari, kwani itasaidia

Dkt. Kezaabu

kufundisha watoto madhara yake na kujua namna ya kujiepusha.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika hoteli moja huko mjini Mbarara nchini Uganda, Dr. Kezaabu amesema watu wengi wameathirika kwa filamu za ngono kupitia njia mbali mbali wanazoweza kuzipata, ingawa walishaahidi kulimaliza kutokana na sheria zilizopo.

Pia Dkt. Kezaabu amesema kwamba Mkurugenzi wa maadili na masuala ya dini wa Ofisi ya Rais, mchungaji Canon Aaron sasa anahamasisha umma kuhusu sheria ya kupinga filamu za ngono, na kuonya kwamba yeyote atakayekiuka atakamatwa na kushtakiwa.