Ijumaa , 20th Mar , 2020

Siku tatu baada ya Jeshi la Polisi nchini, kukamilisha operesheni yake ya pili ya kudhibiti mauaji kwa Mikoa Sita ya Kanda ya Ziwa, watu watatu wameripotiwa kuuawa kinyama akiwemo mama mjamzito wa miezi nane kwa kunyongwa huku wengine wakikatwa mapanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 20, 2020, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo, ambapo amesema kuwa mauaji hayo yametokea katika Wilaya mbili tofauti ikiwemo Masumbwe Wilaya ya Mbogwe, Mji mdogo wa Katoro na Mpomvu wilayani Geita.

Aidha Kamanda Mponjoli amesema kuwa hadi sasa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa hakuna aliyekamatwa kutokana na matukio hayo.