Watu wawili wafariki dunia wakibatizwa

Monday , 17th Jul , 2017

Watu wawili wamefariki dunia wakati wakibatizwa kwenye mto Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro jana Jumapili.

Naibu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Selemani Issa, watu hao walikuwa wakibatizwa kwa kuzamishwa ndani ya maji, shughuli iliyokuwa ikifanywa na Muhubiri wa Kanisa la Shalom huko Rombo.

 

Watu hao walizama kwenye mto Ugwasi wakati wakizamishwa kwa kile kilichoelezwa na Kamanda Issa kuwa ni kuzidiwa na mawimbi makali ya mto huo.

 

Kwa mujibu wa Kamanda Issa, Polisi wameopoa maiti  na kwamba, baadhi ya waumini wa Kanisa na Mhubiri wanazuiliwa kwa mahojiano zaidi.