Jumapili , 17th Mar , 2019

Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole sendeka ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata watumishi 12 akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Iluminata Mwenda kwa ubadhilifu.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Cristopher Ole Sendeka.

Watumishi hao wanadaiwa kuitia hasara serikali kufuatia ubadhilifu wa fedha wa shilingi bilioni 5.5 za ujenzi wa kituo cha mabasi mkoni humo.

Agizo hilo la Mkuu wa Mkoa limekuja kufutia  taarifa ya Mdhibiti na  Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kusema  ujenzi huo  haukufuata taratibu za manunuzi na Kwamba hata mkandarasi aliyepewa zabuni ya  ujenzi huo  hakuwa na sifa  ya kufanya kazi hiyo jambo ambalo limeipelekea serikali hasara.

Aidha katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole sendeka ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama  kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wahusika wote waliokimbia katika kikao cha dharula alichoitisha ili kutoa taarifa za ya Mdhibiti na  Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

Ujenzi wa kituo cha mabasi mkoani Njombe ulianza rasmi mwaka 2018 na kutakiwa kukamilika mapema Januari mwaka, jambo ambalo limekuwa kinyume na mataraji hayo.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.