Jumapili , 10th Nov , 2019

Basi la Kampuni ya Ilasi limeligonga basi la Mbeya Express usiku wa kuamkia leo, katika eneo la Machimbo mkoani Mbeya wilayani Mbarali, huku kukiripotiwa vifo vya watu wawili na majeruhi nane.

Akizungumzia ajali hiyo Mganga Mkuu, Hospitali ya Wilaya ya Mbarali Dr. Godfrey Mwakalila, amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo eneo la Machimbo, ambapo chanzo kikubwa ni uzembe basi la Ilasi ambaye anadaiwa kuendesha kwa mwendokasi.

Shayo amesema kuwa mpaka sasa kati ya marehemu wawili, mmoja mwili wake umeshachukuliwa na ndugu zake, huku mwili mwingine ukiendelea na taratibu za kuutambua.

"Ni kweli ajali hiyo imetokea eneo la Machimbo wilayani Mbarali na watu wawili wamefariki Dunia, na kuna majeruhi 8 na sisi ndiyo hao tumewapokea na mpaka muda huu tunaongea wmwili mmoja wa merehemu umeshachukuliwa na ndugu zake."