Wazazi na Wabunge watakiwa kuwalinda wasichana

Alhamisi , 7th Nov , 2019

Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara, amesema kuwa kwa sasa Serikali inashughulika na kujenga mabweni ya wasichana kwa zile shule zinazochukua wanafunzi wa kitaifa pekee na kuwataka wazazi na wabunge, kuhakikisha wanawalinda wale wasichana wanaosoma shule za kutwa wasipate,

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara.

ujauzito na kukatisha masomo yao.

Waitara ameyabainisha hayo leo Novemba 7, 2019, Jijini Dodoma, katika Bunge la 11, Mkutano wa 17 Kikao cha 3, wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, lililokuwa likibainisha suluba wanazopitia watoto wa kike, hasa wale wanaosoma Shule za kutwa kwa kuiomba Serikali ione umuhimu wa kuwasaidia watoto hao kujengewa mabweni ili waweze kuendelea na masomo na kwamba Serikali itapopata uwezo itajenga.

"Tunayo changamoto ya namna ya kusaidia watoto wa kike, kuwapunguzia suluba wanayoipata ya kwenda Shule na kurudi na jibu la Serikali ni kuwa mnasaidia kwenye Shule ambazo zinachukua wanafunzi wa kitaifa, nyinyi hamuoni kuna haja ya kuwasaidia hawa mabinti zetu ili waweze kupata sehemu ya kukaa na kupata masomo yao?" alihoji Mbunge wa Mtama .

Baada ya swali hilo Naibu Waziri TAMISEMI, Mwita Waitara alitoa majibu, "Tungekuwa na uwezo mkubwa tungejenga mabweni katika Shule za kutwa, maana tunajua ziko karibu na makazi ya wananchi, tumeelekeza wazazi na wabunge kuendelea kuchukua tahadhari ya kulinda watoto wa kike kwa sasa tuna 'deal'na wale ambao wako mbali na makazi yao, tukipata uwezo wa kutosha tutafanya hili" amesema Waitara.

Aidha katika swali lake la pili la nyongeza, Mbunge wa Mtama, alihoji umuhimu wa wakandarasi wa usambazi wa umeme vijijini kuwa suala la uwekaji wa miundombinu ya umeme katika shule zilizoko Vijijini, linapaswa kuwa ni la lazima na si kama sasa ambavyo wanafanya kama hisani.