Jumatatu , 20th Jan , 2020

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, amemteua Godfery Simango Nyaisa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa.

Waziri Bashungwa amemteua Godfery Simango Nyaisa usiku wa kuamkia leo ambapo anachukua nafasi ya Loy Waston Mhando ambaye alikuwa anakaimu nafasi hiyo.

Kabla ya uteuzi huu Godfery Simango Nyaisa alikuwa Mkurugenzi wa Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambapo uteuzi huo umeanza rasmi mara moja kuanzia jana.