Jumapili , 10th Nov , 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema Mamlaka ya Uchaguzi inawatambua wagombea wa vyama vya upinzani vilivyotangaza kujitoa kwenye Uchaguzi huoambao ni CHADEMA na ACT - Wazalendo,

wanaotambuliwa kuwania nafasi zao kutokana na kufuata taratibu za kuchukua fomu.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusiana na mwenendo wa Uchaguzi huo, ambapo amesema mpaka sasa Chama Cha Mapnduzi kimefanikiwa kupitia bila kupingwa katika maeneo mengi zaidi.

"Katika uchaguzi huu hakuna kukimbia wala kuweka mpira kwapani, lazima wote waucheze, wale wote waliochukua fomu na kurejesha lazima washiriki uchaguzi," amesema Jafo

Aidha Waziri Jafo amesema mtu ambaye hana sifa huyo ndiye pekee hataweza kushiriki katika uchaguzi huo, isipokuwa wale waliochukua fomu na kurejesha hata kama chama chake kimetangaza kujitoa, lazima watapigiwa kura.