
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama
Waziri Mhagama ametoa agizo hilo alipokagua shughuli za mradi huo unaotekelezwa katika shamba Na. 217 lililopo eneo la Mkulazi, Morogoro vijijini na kueleza kuwa kamati hiyo kushindwa kutatua changamoto za barabara na umeme kwa wakati, kunasababisha matarajio ya mradi huo ya uzalishaji wa sukari yanashindwa kutimia.
"Maamuzi yalifanyika Novemba na hadi leo Machi hakuna kilichofanyika kwenye kufuatilia, nataka mwezi huu wa tatu kabla haujaisha ujenzi wa barabara uanze na nataka majibu ya lini shughuli za kuweka umeme hapa zinaanza, huu ni mradi wa kimkakati kwani tunao upungufu wa tani 200,000 za sukari ambazo zitazalishwa hapa, kama hakuna kitakachofanyika nitachukua hatua kwenu," amesema Waziri Mhagama
Akieleza changamoto zinazosababisha utekelezaji wa mradi huo usianze, Mwenyekiti wa Bodi ya mradi Dkt. Hildelitha Msita, amebainisha kuwa changamoto ya umeme ni tatizo kubwa lilikuwa ni kwenye makubaliano kati ya mradi na TANESCO juu ya gharama za kujenga njia za umeme huo kwa kuwa njia hiyo haikuwa kwenye bajeti yao.