Alhamisi , 23rd Jan , 2020

Mbunge wa Chemba Juma Nkamia, ameeleza jinsi alivyompambania Mchezaji wa Aston Villa Mbwana Samatta, ili kuhakikisha anatimiza ndoto yake ya kwenda kucheza soka Ulaya.

Mbwana Samatta

Nkamia ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital, ambapo amesema mchezaji huyo mwanzoni alifanyiwa njama ili akose Visa ya kuingia Ulaya.

"Nakumbuka nikiwa Naibu Waziri alihangaika sana kupata visa ya kuingia Ulaya, na nakumbuka aliniambia alizuiliwa kupata visa ya kuingia Ulaya na Ubalozi wa Ufaransa" amesema Nkamia.

"Nakumbuka ikanibidi tusitafutie visa kutokea Ufaransa, ikanibidi niende mpaka Ubalozi wa Hispania ndiyo maana mpaka sasa unamuona yupo huko Ulaya." ameongeza Nkamia.

Hivi karibuni Mchezaji Mbwana Samatta alisaini mkataba wa miaka 4 ndani ya Klabu ya Aston Villa akitokea Genk ya nchini Ubelgiji.